Taarabu ~ Isha Mashauzi (TANZANIA) 2015

Isha Mashauzi ni mwimbaji na mtunzi mahiri wa nyimbo za taarab kutoka nchini Tanzania. Anafahamika sana kwa kuwa mmoja kati ya walioanzisha kundi zima la taarab la Jahazi Modern Taarab. Kundi ambalo linaongozwa na Mzee Yusuf.

Mara yake ya kwanza kupanda jukwaani na kuimba na kundi la Jahazi, ilikuwa kwenye onyesho lililofanyika kwenye ukumbi wa bwalo la maofisa wa polisi, Oysterbay, Dar es Salaam. Katika onyesho hilo, aliimba wimbo wa “Hayanifiki” ambao umempatia umaarufu kwa kiasi kikubwa na kumfanya atambulike kwenye ulimwengu wa muziki wa taarab nchini Tanzania. Tangu hapo, akawa anashiriki kwenye vibao kadha wa kadha. Kibao hicho kilitungwa na Mzee Yusuf.

Miaka miwili baadaye, alifanikiwa kutunga wimbo wake mwenyewe, unaotambulika kwa jina la “Ya Wenzenu Midomo Juu”. Wimbo ambao unapatikana kwenye albamu ya “VIP”, ambayo ni ya nne kwa Jahazi. Wimbo huo ulimfanya awe juu na kuweza kupata mashabiki wengi zaidi kwenye ulimwengu wa mipasho.

**********************************************************************************************************************************************************

Isha Mashauzi is a well known award winning “Taarab” Singer and Composer. “Taarab” is a popular Tanzanian traditional music genre . She is one of the founders of the most popular “Taarab” groups in Tanzania Jahazi Morden Taarab, which is led by the Tanzanian legend Mzee Yusuf.

She performed her first song with the group at the Police Officers Mess Oysterbay, Dar es Salaam, the song titled HAYANIFIKI, the song became very popular and rose her to fame, she went on to sing a lot of songs with the group.

Two years later she started writing her own songs and singing them with the group, she composed good songs which kept her on the list as one of the top female taarab singer. She then decided to do solo projects.